UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe, utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina leo Februari 2, Azam FC inatarajia kumenyana na TP Mazembe kwa ajili ya kujiweka sawa na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa maandalizi yapo tayari na wanaamini watapata matokeo mazuri pamoja na kuimarisha kikosi.
"Kwa timu za Tanzania, ni Azam FC pekee ambayo imeweza kuifunga TP Mazembe ndani ya dakika 90 uwanjani hivyo unaona kwamba rekodi zetu sisi zipo vizuri.
"Julai 16, 2019 kwenye robo fainali ya michuano ya Kombe la Kagame nchini Rwanda, Azam FC tulishinda kwa mabao 2-1.
"Mabao ya Azam FC yaliwekwa kimiani na winga Idd Seleman 'Nado' na mshambuliaji Obrey Chirwa, huku lile la Mazembe likifungwa na Ipamy Giovani.Hapo unaona namna gani tupo vizuri.
"Licha ya kwamba ni mchezo wa kirafiki wachezaji wetu watapambana ili kupata matokeo mazuri na itakuwa ni sehemu ya kazi kwa ajili ya kuelekea kwenye mechi za ligi pamoja na mashindano mengine,"