Mbeya. Diwani wa Ifumbo wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya, Weston Mpyila ameiomba Serikali kuwasaidia kupata ufumbuzi kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa ajabu wa wananchi kutapika damu akidai zaidi ya watu 10 wamefariki dunia na zaidi ya 50 ni wagonjwa.
Ameeleza hayo jana jioni Ijumaa Februari 5, 2021 katika kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya Chunya, kutaka majibu ya Serikali kama inafahamu ugonjwa huo.
Mganga mkuu Wilaya ya Chunya, Felista Kisandu alikiri kuwepo kwa ugonjwa huo na kwamba tayari timu ya idara ya afya imekwenda katika kata hiyo.