Rais wa Marekani Joe Biden alimaliza "Azimio la Dharura la Kitaifa", lililowekwa na mtangulizi wake Donald Trump ambalo lilifungua njia ya ufadhili wa bajeti ya serikali ya ukuta uliojengwa kwenye mpaka wa Mexico.
Katika barua yake aliyoituma kwa Baraza la Wawakilishi na Seneti juu ya suala hilo, Joe Biden alibaini kutohitajika kwa tangazo lililotolewa na Trump na kusema,
"Natangaza kwamba ni sera ya serikali kutotumia ushuru kutoka kwa watu wa Marekani kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa mpakani."
Biden alilijulisha Bunge kwamba Azimio la Dharura la Kitaifa sasa limeondolewa na mamlaka zote zilizopewa ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa kusini zilifutiliwa mbali.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Msemaji wa Pentagon, John Kirby alijibu swali aliloulizwa endapo wanajeshi wa mpakani watajiondoa kufuatia hatua hii iliyochukuliwa na Biden, kwa kusema, "Ufadhili umetengwa kwa ajiil ya wanajeshi hapo mwishoni mwa mwaka. Kwa hivyo hakuna taarifa kuhusu wanajeshi hao kwa sasa."
Rais wa zamani Trump aliamua kujenga ukuta wa chuma unaofunika Arizona, Texas na sehemu ya jimbo la California ili kuzuia wavamizi kutoka mpaka wa Mexico kuingia Marekani.