Rais wa Marekani Joe Biden amesaini awamu nyingine ya maagizo ya kubatilisha amri zilizosainiwa na mtangulizi wake Donald Trump kuhusu uhamiaji.
Maagizo hayo kuhusu kuzitenganisha familia, usalama wa mipaka pamoja na uhamiaji kwa kufuata sheria, yanaongeza idadi ya amri alizosaini kufikia tisa kuhusu uhamiaji wiki mbili tu tangu aingie ofisini.
Biden alitetea hatua zake dhidi ya ukosoaji akisema anachofanya ni kuondoa sera mbaya:Amri aliyosaini Biden kuhusu uhamiaji kinyume cha sheria, inalenga kupunguza mrundikano na vizingiti dhidi ya wanaoomba uraia.