Biden azungumza na Xi kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa





Rais wa Marekani Joe Biden ametumia mazungumzo yake ya kwanza na mwezake wa China Xi Jinping kuelezea wasiwasi wa Washington juu ya ukiukaji wa haki za binadamu kwenye jimbo la Xinjiang na tabia ya mabavu inayotumiwa na China katika shughuli za uchumi.
 Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Marekani imesema katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jana, Biden pia amezungumzia ukandamizaji unaofanywa na China kwenye mji wa Hong Kong na mwenendo wa nchi hiyo kwenye kanda ya Asia ikiwemo kuhusu suala la Taiwan. 

Kwa upande wake Xi ametumia mazungumzo hayo kumuonya Biden kujiepusha na uhasama ambao amesema unahatarisha ustawi wa nchi hizo mbili na ulimwengu kwa jumla. 

Kulingana na shirika la habari la China, Xinhua, rais Xi amemtaka Biden kuheshimu maslahi ya Beijing ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari anaposhughulikia masuala ya Hong Kong, Taiwan na Xinjiang akisema hayo ni mambo ya ndani ya China.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad