Bongo Flava ya Sasa ni uozo Mtupu..Tungo za Matusi na Ngono Zatawala


Ameandika Penologist

Salaaam wakuu,

Nimekuwa nikisikiliza mziki wa bongo flava kuanzia enzi za takeu ikaja kiduku, ikaja ngololo hadi kufikia mpelekee moto.


Ukweli ni kwamba hapo nyuma walianza vizuri kwa upande wa hiphop kina niger j na Mr.2 wakatengeneza njia wakaandika mashairi ya kuelimisha jamii na wengine waka fanya hiphop cartoon ambayo inaelimisha na kuburudisha. Watu tukaelewa mziki wa bongo tukasikiliza hadi sitting room tukiwa familia nzima.


Kwa upande wa bongo flava tulisikiliza tungo nzri za mapenzi kina T.I.D,Matonya,Mb doggy na Mr.Nice waliandika nyimbo za mapenzi zenye staha unazoweza sikiliza na familia watu tukauelewa mziki wa bongo.

Wakaendelea vizuri ukaja mziki wa kucheza wenye tungo hafifu lakini hakuna matusi, tuta wakumbuka kina msami, mesen selecta, diamond wa number one, Ali wa chekecha, shetta wa kerewa na wengine.


Miaka ya hivi karibuni sasa ndiyo imekuwa tatizo mziki ni matusi na ngono mubashara tungo zimekuwa explicit yaani unaogopa hata kusikiliza ukiwa pekeyako licha ya kuwa na familia, mziki uliotawaliwa na tungo za ngono tupu, mziki usiokuwa na staha, kila upande ni vurugu siyo hiphop wala bongo flava, maneno utakayo sikia ni mpelekee moto Hugo ni baddest, yupo young lunya atakuambia habari za kupeleka moto hadi kukojoza mara mpe tango,lulu diva ata kuambia anapenda Mandingo ina mkolea kitandani utasikia napenda inavyo zama. Tpuu naona aibu ata kuandika hapa.


Mziki wa bongo flava umekuwa kielelezo cha maadili kuporomoka kwa kiwango cha sgr. Rai yangu kwa basata fungieni huo uozo ata kama zikitoka nyimbo chache zenye heshima ni bora mpaka pale wasanii watakapo jifunza kuandika tungo zenye maadili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad