Dawa 46 za tiba asili zasajiliwa Tanzania

 


Dawa 46 za tiba asili zimesajiliwa na msajili wa baraza la tiba asili Tanzania baada ya kuhakikiwa na mkemia mkuu wa Serikali.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Februari 2, 2021 na msajili wa baraza la dawa asili na tiba mbadala, Dk Ruth Suza wakati akitoa taarifa za masuala ya tiba asili kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Dk Suza amesema dawa hizo zimehakikiwa na mkemia mkuu wa Serikali na kukidhi vigezo vya ubora na usalama na binadamu akizitumia haziwezi kumletea madhara.

“Utaratibu wa usajili wa dawa unaanzia idara ya mimea kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam baada ya hapo dawa husika hupelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali kuangalia ina vigezo gani. Wakishapima itaamuliwa kwamba inaweza kupimwa iwapo ipo salama kwa kuangalia sumukuvu kuhakikisha ubora kwa matumizi ya binadamu,” amesema Dk Suza.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad