Idara ya FDA nchini Marekani yaidhinisha matumizi ya dawa mpya dhidi ya virusi vya ukimwi
1569284
Dawa mpya ya VVU yaboreshwa
Idara ya Chakula na Dawa nchini Marekani (FDA), imeidhinisha dawa aina ya "Cabenuva" iliyoundwa dhidi ya virusi vya Ukosefu wa kinga ya mwili (VVU) kutumika mara moja kwa mwezi.
Maafisa wa Marekani walitangaza kwamba idara hiyo ya FDA imeidhinisha dawa inayoitwa "Cabenuva", ambayo inaingizwa mwilini kwa sindano mara moja kwa mwezi na ina athari ya muda mrefu zaidi kama kinga mbadala kuliko vidonge vya kila siku vinavyotumiwa na watu wenye VVU.
"Cabenuva" imebreshwa kutokana na ujumuishaji wa "Rilpivirine" iliyozalishwa na kampuni ya Johnson & Johnson na "Cabotegravir" iliyozalishwa na ViiV Healthcare.
Ilielezwa kuwa FDA ilitoa idhini ya matumizi ya dawa hiyo mahsusi kwa kwa watu wazima wenye VVU na wagonjwa wasiokuwa na kinga ya kutosha ya kudhibiti virusi.
Cabenuva inatarajiwa kurahisisha ufuatiliaji wa maisha binafsi ya wagonjwa na kulinda faragha zao.
Mtaalamu wa VVU kutoka chuo kikuu cha California Dr. Steven Deeks, alisema dawa hiyo ya "Cabenuva" itaboresha hali ya maisha ya wagonjwa walioambukizwa VVU.