Dkt. Tulia: Nimeugua Corona, Kutokuvaa Barakoa Sio Sababu

 

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa amewahi kuugua ugonjwa wa corona mara mbili hivyo anaufahamu vizuri namna unavyotesa watu.

 

Dkt. Tulia amesema hayo wakati wa ibada ya maziko ya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Likwelile nyumbani kwake, Mpiji Majohe jijini Dar es Salaam, jana Jumanne, Februari 23, 2021.

 

“Ninaifahamu vizuri corona, nimeshaumwa corona mara mbili, lakini kutokuvaa kwangu barakoa haimaanishi kwamba sijilindi wala namuogopa mtu la hasha, kila mmoja ana njia zake za kujilinda. Si kwamba anayevaa barakoa ndiye anajilinda zaidi ya mwingine la hasha.

 

 

“Mimi nikivaa barakoa siwezi kupumua vizuri, wengine wameshauriwa na madaktari wasitumie barakoa kutokana na matatizo ya kiafya waliyo nayo. Tunajilinda na kwa wivu kabisa kwa sababu miili yetu ni hekalu la Mungu.

 

“Kila mtu atakufa, haijalishi utakufa kwa kifo gani lakini kila nafsi itaonja mauti, lakini tunachokitamani zamu yetu isiwe karibu, isiwe sasa, lakini ukweli ni kwamba kila mmoja atakufa, hivyo tukiwa hai hapa duniani tujitahidi kuishi kwa kumpendeza Mungu na watu wanaotuzunguka kwa sababu Mungu amewaumba kwa mfano wake,” amesema Dk.t Tulia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad