Elon Musk Apoteza Taji la Tajiri Zaidi Duniani




ELON MUSK  amepoteza taji lake la kuwa mtu tajiri zaidi duniani baada ya thamani ya hisa za kampuni yake ya Tesla  inayotengeneza magari duniani kushuka.

 

Hisa za Tesla, kampuni la kutengeneza magari, vifaa vya umeme na masuala ya nishati,  zimeshuka kwa zaidi ya asilimia 20 tangu zilipopanda kwa zaidi ya $880 mapema mwezi Januari. Zilishuka kwa kiwango kikubwa wiki hii kufuatia hatua ya kampuni hiyo kuwekeza hivi majuzi $1.5bn (£1bn) katika sarafu ya kidijitali ya Bitcoin.

 

Kushuka kwa thamani ya Musk kunamrudisha Jeff Bezos katika orodha ya mtu tajiri zaidi duniani.

 

Hatari ya kuhusishwa na sarafu ya Bitcoin – ambayo thamani yake imeshuka kwa kiwango kikubwa hivi majuzi huenda ndiyo iliwashinikiza baadhi ya wawekezaji wa Tesla kuuza hisa zao licha ya kwamba kampuni hiyo ilikuwa haijaathiriwa na kushuka kwake, alisema mchanganuzi wa kampuni ya Wedbush Securities Dan Ives.

 

Uuzaji wa sarafu ya Bitcoin katika saa 48 zilizopita na utata unaokumbwa na sarafu hiyo umewafanya baadhi ya wawekezaji kujiondoa.



 

Ni nini kinachosababisha uuzaji wa Bitcoin?

Thamani ya Bitcoin ilipanda kwa asilimia 50 katika wiki zilizopita baada ya Tesla kufichua kwamba iliwekeza $1.5bn katika sarafu hiyo na kupanga kuikubali kama sarafu inayoweza kutumika katika malipo. Lakini tangu ilipopanda juu ya $57,000 siku ya jumapili , sarafu hiyo ya kidijitali imeshuka thamani kwa asilimia 20%. Ilikuwa inauzwa chini ya $48,000 siku ya Jumanne – bado ikiwa ni juu ya wakati Tesla ilipowekeza.

 

 

Je ni nini chengine lkinachoiathiri Tesla?

Bwana Musk ameipatia Muda mwingi Bitcoin wakati ambapo Tesla inakabiliwa na changamoto nyingine. Kampuni hiyi hivi majuzi ilisitisha muazo mengi ya gari jipya aina ya Y SUV , huku bwana Musk akiwa na lengo la kuimarisha muundo wa gari hilo.

 

 



 

Wapinzani wa kampuni hiyo ya magari kama vile General Motors na Volkswagen wameanza kufikiria kuunda magari ya kutumia umeme katika miezi ya hivi karibuni. Hatua hiyo inafuatia kupanda kwa hisa za Tesla 2020 ambapo bei zake zilipanda kutoka $90 hadi $700.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad