Fahamu vyanzo vya utajiri wa Aliko Dangote na Mohammed Dewji pamoja na mabilionea wengine wa Afrika

 


Kwa mujibu wa jarida la Forbes mwaka 2021, utajiri wa Mabilionea kutoka bara hili uliongezeka kwa asilimia 12 zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Hivyobasi tunaangazia vyanzo vya mali walionayo na utajiri wao kwa jumla kwa mujibu wa Forbes.


1.Aliko Dangote ana thamani ya $12.1b.


Mtu tajiri zaidi barani Afrika ndiye mwanzilishi wa kampuni ya simiti ya Dangote , ambayo ndio kubwa zaidi barani Afrika. Anamiliki asilimia 85 ya hisa za kampuni hiyo kupitia kampuni shikilizi. Kampuni ya simiti ya Dangote huzalisha tani milioni 45.6 kila mwaka na inaendeleza operesheni zake katika mataifa 10 barani Afrika. Dangote pia anamiliki hisa katika biashara ya chumvi na sukari. Kampuni ya kusafisha mafuta ya Dangote imekuwa ikijengwa tangu 2016 na inatarajiwa kuwa miongoni mwa kampuni kubwa za kusafisha mafuta duniani itakapokamilika.


2.Nassef Sawiris ana thamani ya $8.5b


Ni mwekezaji anayetoka katika familia tajiri nchini Misri. Mali yake kubwa ni asilimia 6 ya hisa za kampuni ya kutengeneza sare za michezo ya Adidas. Mnamo mwezi Disemba 2020, alifanikiwa kumiliki asilimia 5 ya hisa za kampuni ilioorodheshwa katika soko la hisa la New York ya Madison Square Garden Sports, inayomiliki timu ya mpira wa vikapu ya Knicks na NHL Rangers. Anasimamia OCI, mojawapo ya wazalishaji wakuu wa mbolea , ikiwa na kampuni katika majimbo ya Texas na Iowa. Imeorodheshwa katika soko la hisa la Euronext Amsterdam. Kampuni ya ujenzi ya Orascom , kampuni ya uhandisi na ujenzi, ipo katika soka la hisa la Cairo na Nadaq Dubai. Kampuni zake zina hisa katika kampuni kubwa ya simiti ya Lafarge Holcim na Adiddas. Anaketi katika bodi ya kusimamia Adidas.


3.Oppenheimer ana thamani ya $8b


Akiwa mrithi wa mali ya familia yake , aliuza asilimia 40 ya hisa za kampuni ya almasi ya DeBeers kwa kampuni ya Anglo American kwa $5.1b mwaka 2012. Ni mmoja wa watu wa kizazi cha tatu cha familia hiyo kusimamia kampuni ya DeBeers na kuifanya kuwa ya kibinafsi 2001. Kwa miaka 85 hadi 2012, familia ya Oppenheimer ilijipatia sifa kubwa katika biashara ya almasi duniani. Mwaka 2014, Oppenheimer ilianza kufanya kazi katika kampuni ya Fireblade Aviation mjini Johannesburg, ambayo ilikuwa inaendesha ndege za kubeba abiria ikiwa na ndege 3 na helikopta 2. Anamiliki maili 720 mraba za ardhi ya uhifadhi nchini Afrika Kusini, Botswana na Zimbabwe.


Kiwanda

4.Johann Rupert ana thaman ya $7.2b


Ni mwenyekiti wa kubeba mizigo ya burudani ya kampuni ya Uswizi Compagnie Financiere Richemont. Kampuni hiyo inajulikana kwa chapa ya Cartier na Mont blanc. Ilianzishwa mwaka 1998 kupitia mali kadhaa zilizokuwa zikimilikiwa na kampuni ya Rembrandt Group Limited (now Remgro Limited), ambayo babake aliianzisha miaka ya 1940. Anamiliki asilimia 7 ya hisa za kampuni ya uwekezaji ya Remgro, ambayo yeye ndiye mwenyekiti pamoja na asilimia 25 za hisa za Reinet - kampuni ya uwekezaji ilio na makao yake makuu mjini Luxembourg.


5.Adenuga ana thamani ya $6.7b


Mtu wa pili kwa utajiri nchini Nigeria alijitengezea utajiri wake kupitia sekta ya mawasiliano ya simu ya telecom na uzalishaji wa mafuta. Kampuni yake ya simu Globacom ndio ya tatu kwa ukubwa nchini Nigeria ikiwa na wateja milioni 55. Kampuni yake ya uchimbaji mafuta ya Conoil Producing inafanya operesheni katika visima sita vya mafuta katika eneo la Niger Delta. Adenuga anamiliki shahada ya uzamili ya usimamizi wa Biashara katika chuo kikuu cha pace mjini New York , akijisomesha mwenyewe wakati akifanya kazi kama dereva wa teksi. Alijipatia milioni yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 26 wakati alipokuwa akiuza lesi na vinywaji baridi.


6. Abdulsamad Rabiu ana thamani ya $ 5.5b


Ndiye mwanzilishi wa kundi la kampuni za BUA , msururu wa kampuni zinazozalisha simiti, sukari, na ujenzi na uuzaji wa nyumba. Mapema mwezi Januari 2020, Rabiu aliunganisha kampuni yake ya kibinafsi ya Obu Cement na kampuni ilioorodheshwa katika soko la hisa ya Cement Co kutoka kaskazini mwa Nigeria ambayo aliidhibiti. Uunganishaji wa kampuni hizo mbili ulizalisha kampuni ya BUA Cement Plc ambayo inafanya biashara ya hisa katika soko la hisa la Nigeria ambapo Rabiu anamiliki asilimia 98.5 za hisa zake. Rabiu, mwana wa mfanyabiashara , alirithi ardhi kutoka kwa babake. Alianzisha biashara yake mwenyewe 1988 akinunua kutoka nje mabati, chuma na kemikali.



7. Issad Rebrab ana thamani ya $4.8b


Ndiye mwanzilishi afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Cevital, kampuni kubwa nchini Algeria . Cevital inamiliki kampuni kubwa ya sukari duniani ikiwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni 2 za sukari kila mwaka. Cevital pia inamiliki makampuni ya Ulaya ikiwemo kundi la kampuni za kuuza vitu vya nyumbani Brandt, kampuni moja ya kutengeneza vyuma nchini Itali na kampuni nyengine ya kusafisha maji ya Ujerumani.


8. Naguib Sawiris ana thamani ya $3.2b


Anatoka katika familia tajiri nchini Misri. Ndugu yake Nassef pia ni bilionea. Alijipatia utajiri wake katika mawasiliano ya simu kwa kuuza kampuni ya Orascom Telecom mwaka 2011 kwa kampuni ya mawasiliano ya simu nchini Urusi VimpelCom (sasa ikijulikana kama Veon) katika mazuo yalioshirikisha mabilioni ya madola. Ni Mwenyekiti wa kampuni ya uwekezaji ya Orascom TMT, ambayo ina hisa na mali nchini Misri pamoja na kumiliki kampuni ya Intaneti nchini Itali , Italionline miongoni mwa nyenginezo. Kupitia kampuni yake ya Media Globe Holdings, Sawiris anamiliki asilimia 88 ya huduma ya televisheni ya malipo na kampuni ya habari ya Euronews. Pia alitengeneza eneo la kifahari la burudani la Silversands katika kisiwa cha Caribbean cha Grenada.


9. Patrice Motsepe ana thamani ya $ 3b


Ni mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya African Rainbow Minerals, ambapo alikuwa bilionea mwaka 2008 - akiwa mwafrika wa kwanza kuorodheshwa katika orodha ya jarida la Forbes. Mwaka 2016 , alizindua kampuni ya kibinafsi African Rainbow Capital ilioangazia uwekezaji barani Afrika. Motsepe pia anamiliki hisa katika kampuni ya Samlam, kampuni ya huduma za fedha ilioorodheshwa katika soko la hisa na ni rais na mmiliki wa klabu ya soka ya Mamelodi Sundowns . Mwaka 1994, alikuwa mwanzilishi mwenza wa kwanza mweusi katika kampuni ya mawakili ya Bowman Gilfillan mjini Johannesburg, na baadaye alianzisha biashara ya huduma za kutoa kandarasi za uchimbaji madini. Mwaka 1997, alinunua mashine za uchimbaji madini wa kiwango cha chini na baadaye kuziuza ambapo alijipatia faida kubwa.


10 .Koos Bekker ana thamani ya $2.8b


•Anasifiwa kwa kubadili kampuni ya kuchapisha magazeti Nasper kuwa mwekezaji wa kibiashara na runinga. Aliiongoza Nasper kuwekeza katika intaneti ya China na kampuni ya habari ya Tencent mwaka 2001 - Huo ndio uwekezaji uliompatia fedha nyingi zaidi ugenini. Mwaka 2019, Nasper iliwekeza mali yake katika kampuni mbili ambazo hisa zake zilikuwa zinauzwa kwa raia , kampuni ya burudani ya Multichoice Group na Prosus ambayo inamiliki hisa za Tencent. Iliuza asilimia 2 ya hisa za Tencent mwezi Machi 2018 , kwa mara yake ya kwanza ikipunguza hisa zake , lakini ikasema wakati huohuo kwamba kamwe haitauza hisa hizo kwa kipindi cha miaka mitatu. Bekker ambaye alistaafu kama afisa mkuu mtendaji wa Naspers mwezi Machi 2014 alirudi kama mwenyekiti wake mwezi Aprili 2015.


13.Mohammed Dewji ana thamani ya $1.6b


Mohammed Dewji

Ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL, kundi la makampuni yalioanzishwa na baba yake 1970. METL inashiriki utengenezaji wa nguo, unga wa ngano, vinywaji na mafuta ya kupikia katika eneo la mashariki, kusini na katikati mwa Afrika. METL inafanya operesheni zake katika mataifa sita ya Afrika na ina mpango wa kupanua operesheni hizo katika mataifa mengine. Dewji, ambaye ndiye Mtanzania wa pekee Bilionea alitia saini mpango wa Giving Pledge 2016. Akiahidi kuchangisha nusu ya mali yake kwa wahisani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad