Gwajima "Kwa Sasa Wizara Haina Mpango wa Kuagiza Chanjo ya Corona"


 “Kufuatia kuwepo kwa taarifa za uwepo wa mlipuko wa pili wa ugonjwa wa Corona katika Nchi Jirani, nimekuwa nikipokea maswali mengi, Watu wakiuliza iwapo Wizara ina mpango wa kupokea chanjo ya Corona na njia zipi zitumike kujikinga na ugonjwa huo,"


“Kwa sasa Wizara haina mpango wa kupokea chanjo ya Corona inayoripotiwa kuwepo na kutumika kwenye Mataifa mengine, ifahamike kuwa Serikali kupitia Wizara inazo taratibu zake za kufuata inapotaka kupokea bidhaa yoyote ya afya na kufanyika baada ya kujiridhisha, hivyo kwa nia njema kabisa ni hadi tujiridhishe na sio vinginevyo,"


“Kuhusu mbinu za kujikinga na Corona, Wananchi wajielekeze kwenye Elimu inayotolewa na Wataalamu wa Afya ikiwemo kuimarisha usafi wa mazingira na wa Mtu mmojammoja, kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, sanitizer,Lishe,kujifukiza,mazoezi na matumizi ya Tiba asili,"


“Nazikumbusha Taasisi zote za Umma, Taasisi za Kidini, Taasisi Binafsi, Taasisi za Kijamii na Vyombo vyote vya Habari kuepuka kutoa taarifa za Afya ambazo hazifuati miongozo ya Wizara, wakishatoa taarifa hizo zinazua taharuki na hofu kwa Jamii” - Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na waandishi wa habari Leo jijini Dodoma


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad