Hakuna mgonjwa wa corona hospitali za Bugando, Sekou-Toure




Serikali ya Tanzania imesema hakuna wagonjwa wa corona  katika hospitali ya Kanda ya Bugando na ile ya rufaa ya Sekou-Toure za jijini Mwanza.


Hayo yameelezwa leo  Ijumaa Februari 5, 2021 katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Mabula Mchembe katika mkutano wake na waandishi wa habari huku akiwataka wananchi kutokuwa na hofu.



Katibu mkuu huyo alitembelea hospitali hizo ili kupata ukweli kama zina wagonjwa hao  ama la baada ya madai hayo kusambaa mitandaoni kuanzia juzi.



Awali akitoa taarifa kwa katibu mkuu huyo, kaimu mkurugenzi wa Bugando, Dk Fabian Massaga amesema hospitali hiyo haina mgonjwa yeyote wa Covid 19 kama inavyodaiwa.



Amesema wagonjwa wanaopokelewa ni wale wenye changamoto ya kupumua inayotokana na maradhi mengine ikiwemo shinikizo la damu, uzito uliopitiliza na kifua kikuu.



Maelezo kama hayo pia yalitolewa na mganga mfawidhi wa Sekou-Toure, Dk Bahati Msaki, “tunao wagonjwa watano wenye changamoto ya kupumua inayotokana na maradhi mengine.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad