Halmashauri ya Meru na wananchi waingia katika mgogoro kugombea ardhi ya EPZ





Halmashauri ya Meru, wilayani Arumeru, imeingia katika mgogoro wa kugombea ardhi, ekari 2,456 Katika kijiji cha Malula zinazomilikiwa na wananchi ikitaka zitumike kujengwa Ukanda wa uwekezaji(EPZ).


Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa wamiliki wa maeneo hayo, Sophia Okash alisema wanamiliki eneo la hekari 2,456 tangu mwaka 1954, anashangazwa na Halmashauri ya Meru kuvamia shamba hilo na kuanza kuweka alama wakati wakijua sio mali yao.



Alisema kulikuwa na shauri la madai ya ardhi namba 35 la mwaka 2012 katika mahakama kuu Arusha kati yake kama msimamizi mirathi ya Baba yake, Ahmed Okash na watu 82 waliokuwa wamevamia na uamuzi ukatolewa Februari 14, mwaka jana na Jaji Yohanne Massara na nikashinda kesi kuwaondoa wavamizi .



Alisema baada ya kushinda kesi hiyo, anashangaa halmashauri ya Meru, kuvamia eneo lao na kuanza kuweka alama na kudai ni mali ya serikali kwa maelezo ambayo sio kweli kuwa baba yake alipangishwa mwaka 1973/74.



Alisema sio kweli kuwa mzazi wake alipangishwa eneo hilo mwaka 1974 kwani alifariki tangu mwaka 1969 na kuacha eneo hilo likiwa ni shamba na mali mbali mbali.



“Baada ya kufariki Mzee kuna waliokuwa viongozi wa hamalshauri na wa kisiasa walivamia eneo letu na kuanza kulima Kwa nguvu na ndio hao tumewashinda kesi,”alisema



Mkurugenzi wa halmashauri ya Meru, Emmanuel Mkongo, akielezea eneo Hilo ni na mengine jirani yanayofikia hekali 4,086 ni mali ya serikali na anachofahamu ni kuwa serikali iliwapangisha wananchi eneo hilo kwa kilimo mwaka 1973 na 1974.



Hata hivyo, Katika eneo pia bado kuna kesi nyingine mahakamani ya kuu ya mmiliki mwingine wa heka 1,000 Gabriel Mmari akipinga kuvamiwa eneo lake.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad