Hii ndio orodha mpya mataifa 25 yenye nguvu ya kijeshi duniani




Jarida la kimataifa la ‘Firepower’ ambalo huwa linalinganisha uwezo wa vikosi vya majeshi duniani kila mwaka , limetoa orodha ya mataifa 138 pamoja nguvu walizo nazo.



Ripoti hiyo imeangalia idadi ya silaha, jeshi na rasilimali fedha ambazo nchi hizi hutumia katika operesheni za kijeshi.

Nafasi ya kwanza katika orodha huwa haibadiliki kila mwaka . Ingawa baadhi ya nchi huwa zna uwezo tofauti kila mwaka.

 

Mataifa manne ambayo hayajabadilika katika nafasi zake kwa miaka ya hivi karibuni ni pamoja na :

1- Marekani

2- Urusi

3- China

4 India

Uturuki ikiwa imeshuka
Wanajeshi wa Uturuki
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka huu uanze, Uturuki imekuwa ikishuka katika orodha ya mataifa kumi bora yenye majeshi yenye nguvu.Lakini Misri imeweza kufikia kumi bora, na kuiweka miongoni mwa taifa lenye jeshi bora zaidi duniani.

Barani Afrika, taifa la Misri ndilo linaloongoza huku likiwa katika nafsi ya tisa ulimwenguni

Mataifa mengine ni:
5- Japan

6- Korea Kusini

7- Ufaransa

8- Uingereza

9- Misri

10- Brazil

Kwa miaka miwili iliyopita, Uturuki ilikuwa inachukua nafasi ya tisa wakati miaka mingine ya nyuma taifa hilo lilikuwa nafasi ya nane, lakini mwaka huu imekuwa ya 11.

Ushawishi wa Saudia
Karibu mataifa yote 25 ya mwanzo hayajafanya mabadiliko makubwa .
Karibu mataifa yote 25 ya mwanzo hayajafanya mabadiliko makubwa .
Baadhi yameshuka viwango kidogo wakati mengine yakiwa hayana ongezeko lolote .

Lakini miongoni mwa mabadiliko makubwa zaidi kwa mwaka huu ni Saudi Arabia kuwa miongoni mwa orodha ya juu zaidi kwa mara ya kwanza.

Himaya hiyo inayoongozwa na mfalme Salman bin Abdulaziz imefika namba 17 huku Israel ikiwa namba 18 katika orodha ya mataifa yenye nguvu zaidi duniani.

Mwaka 2016, Saudi Arabia ilikuwa namba 24 huku Israel ikiwa inashika namba 16 katika orodha.

Mwaka uliofuata, 2017, Saudi Arabia ilibaki kuwa nafasi ya namba 24th huku Israel ikiwa nafasi ya 15.

Mwaka 2018, Saudi Arabia ilitoka katika orodha ya 25 bora lakini Israel ilishika nafasi ya 16.

Mwaka jana 2019, Saudi Arabia ilijitahidi mpaka ikachukua nafasi ya 25 wakati Israel ikiwa nafasi ya 17.
Mwaka jana 2019, Saudi Arabia ilijitahidi mpaka ikachukua nafasi ya 25 wakati Israel ikiwa nafasi ya 17.
Mataifa bora 25 katika orodha ni pamoja na :
11- Uturuki

12- Italia

13-Ujerumani

14-Iran

15- Pakistan

16- Indonesia

17- Saudi Arabia

18-Israel

19- Australia

20- Hispania

21- Poland

22- Vietnam

23- Thailand

24- Canada

25. Korea Kaskazini


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad