Kuna Faida Simba watapata kama klabu. Kuna faida nchi itapata na kubwa zaidi, hii project ina Faida kubwa pia kwa mpira wetu
Kivipi? Mechi 6 za hatua ya makundi kwa makadirio inaweza kupata viewers zaidi ya 500M kutoka sehemu mbalimbali duniani
Na hii ni kutokana na Tathimini ya baadhi ya TV Channels zitakazoonyesha mechi hizi
Canal Algérie, BeIN Sports, Eurosport, ESPN, Arryadia, GTV ya Ghana,
MENA beIN Sports na West Africa Canal+
Kwa neno 'VISIT TANZANIA' mbele ya jezi ya Simba litatangaza Utalii wetu Tanzania kupitia Channels hizo kwa kila dakika 90 Simba atakazoshuka dimbani (Iwe Misri, Sudan na Tanzania)
Watalii wengi wanaoingia nchini wanatoka nchi za Ulaya na America, kupitia Channel za SportFive (ULAYA) na BeinSports (USA) zitakazorusha mechi za hatua ya makundi, kundi hilo kubwa litakuwa limefikiwa
Tutavuta watalii wengi kuifatilia nchi yetu kwa kuitumia jezi ya Simba tu
Iko mifano mingi ya nchi zilizofanikiwa sana kwenye sekta hiyo kwa kuutumia mchezo wa mpira wa miguu
Serikali ya Rwanda ilithubutu hili kwa kuliweka neno 'VISIT RWANDA' kwenye jezi ya Arsenal na ripoti ilionyesha pato lao la Utalii lilikuwa kwa asilimia 5 baada ya project hiyo
Simba wametumia vyema fursa ya LIGI YA MABINGWA kuongeza Thamani ya Brand yao
Unaweza kujiuliza kwanini SPORTPESA wameondoka? Jibu ni rahisi tu, CAF tayari wana udhamini wa kampuni ya XBET
Hivyo kanuni haziruhusu. Simba wangeweza kwenda jezi ikiwa njeupe mbele. Lakini kwanini wafanye hivyo? Akili kubwa ikaingia kati
Wameipa pia thamani nchi yetu kwenye sekta ya Utalii na sio kuwaza heshima ya nchi kwa kushinda tu uwanjani
Pia project hii ni ishara ya kupanda Thamani kwa mchezo wa mpira wa miguu.
Ni bahati sasa klabu zetu zimeanza kupata viongozi wenye uweledi/wabunifu wanaoweza kufikiria mambo makubwa ndani na nje ya kiwanja
Bravo Simba SC📌