Hizi zinaweza kuwa habari njema kwa Chris Brown kwani ex wake, Karrueche Tran ameripotiwa kuachana na Victor Cruz. Wawili hao ambao wamedumu kwenye mapenzi kwa miaka 3, wameripotiwa kuachana huku kila mmoja akiendelea na maisha yake.
"Kwa sasa, wamejikita kwenye kukuza kazi zao." alisema ripota wa mtandao wa E! News. "Hakuna chuki kati yao, ni suala la watu wawili kuendelea na maisha yao kila mmoja kivyake."