Jeshi la Uganda lakemea ujumbe wa vitisho mitandaoni




Jeshi la polisi nchini Uganda limeonya watu wanaosambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wakitishia wananchi na kuleta hofu nchini humo.
Ujumbe huo ulianza kusambwa mwishoni mwa juma, ambapo ulitaka watu wabaki nyumbani kwa siku tatu ujumbe ambao wameuita 'National Shut down'.

Ujumbe huo unawaonya wananchi kuanzia Februari 03 hadi tarehe 7 Februari wasalie nyumbani kwao bila kufanya kitu chochote.

Naibu wa jeshi la polisi nchini humo IGP Meja Jenerali Paul Oketch ametowa onyo kwa watu aidha makundi yanayosambaza vitisho hivyo kuacha mara moja kuwatisha wananchi la sivyo watachuliwa hatua kali za kisheria.

Vitisho hivi vinakuja wakati taifa hilo likiwa na mgawanyiko wa kisiasa tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa rais baada ya Rais Museveni kutangazwa na Tume ya uchaguzi kuwa mshindi na kuongoza taifa hilo kwa muhula wa sita.

Ingawa Jumatatu kiongozi wa chama cha NUP Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine aliwasilisha kesi mahakama ya juu kupinga ushindi wa Rais Museveni.

Hata hivyo kumekuwa na msukumo toka kwa baadhi ya viongozi wa dini wakiomba Rais Museveni kufanya maridhiano na viongozi wa upinzani kwa maendeleo ya taifa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad