Jeshi la Yemen limetangaza kumuua kamanda mmoja wa Houthis pamoja na watu wengine kadhaa wanaohusika na vikosi hivyo vya kijeshi katika eneo la Hudayda Magharibi mwa nchi.
Katika maelezo yaliyotolewa na makamanda wa Amalika wa jeshi la Yemen, iliarifiwa kuwa mashambulizi ya wanamgambo wa Houthis yalitibuliwa na kuzuiwa na jeshi katika eneo la “Kilo 19” Mashariki mwa Hudayda.
Kamanda wa Houthis Ibrahim Al-Deylemi pamoja na wanamgambo kadhaa waliuawa walipokuwa wakitaka kuingia kwenye ngome za mawasiliano katika eneo hilo.
Kundi la Houthis halijatoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo.
Serikali na viongozi wa Houthis walikutana mjini Stockholm nchini Usiwidi Desemba 2018 kwa ajili ya mazungumzo ya kumaliza mzozo na kutia saini makubaliano ingawa bado kumekuwa na mvutano katika eneo la Hudayda kutokana na tuhuma zinazoendelea kati ya pande zote.