Rais wa Marekani Joe Biden amefanya mazungumzo ya simu na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kuelezea hamu ya Marekani kushirikiana na nchi ya Kenya.
Kulingana na Ikulu ya White House, Biden amesisitiza umuhimu wa uhusiano thabiti kati ya Marekani na Kenya wakati wa mazungumzo hayo.
Kwa mujibu wa habari, Marekani imesisitiza azma yake ya kufanya kazi kwa karibu na Kenya kukuza amani na usalama wa eneo.
Taarifa hiyo ilisema,
"Rais Biden amesifu uongozi wa Kenya, kujitolea kwake kupambana na ugaidi, ukuaji wa uchumi, mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo endelevu,"
Viongozi hao wawili pia walizungumzia mgogoro wa katika mkoa wa Tigray wa Ethiopia.