CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba wana nafasi ya kufanya vizuri ikiwa wachezaji wataamua kujituma.
Kikosi cha Simba chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes kina kazi ya kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa kikiwa kimetinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa huku Namungo nayo pia ikiwa kwenye hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kaze amesema kuwa wawakilishi wote wanapaswa kupewa sapoti kutoka kwa mashabiki huku wachezaji wao wakitakiwa kujituma zaidi ndani ya uwanja kusaka matokeo chanya.
Kaze amesema:"Simba ina wachezaji wazuri na wenye uzoefu wa kutosha kama wataamua kupambana watafika mbali kwenye mashindano ya Kimataifa (Caf Champions League)
"Ikiwa wataanza vizuri wana nafasi ya kufuzu robo fainali kama wachezaji wataamua kujituma na kupambana kwa ajili ya kutafuta matokeo kwenye mechi za makundi.
"Kufanya kwao vizuri kwenye hatua ya makundi, kutafungua faida kwa taifa kiujumla kwani kupanda kwa viwango vya timu ni faida ya taifa kiujumla.
"Hata Namungo pia inaweza kufanya jambo kubwa kwenye mashindano ya kimataifa kwani nafasi ipo wazi ikiwa wachezaji wataamua kujituma bila kuchoka,"