Kocha Simba Amkingia Kifua Morrison





KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amemtetea kiungo mshambuliaji wake, Bernard Morrison kutokana na nyota huyo kuonekana akikosa nafasi nyingi za wazi hasa katika mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji.

 

Katika mchezo huo uliochezwa Alhamisi ya wiki hii ambao Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-0, licha ya Morrison kuhusika katika mabao yote mawili, akiasisti na kufunga, lakini alionekana kupoteza nafasi nyingi za wazi za kuifungia Simba.

 

Akizungumza na Spoti Xtra,Gomes alisema: “Tulikuwa na mchezo mzuri dhidi ya Dodoma Jiji, ni wazi tulistahili kushinda kutokana na nafasi nyingi ambazo tulizitengeneza katika mchezo huo, lakini kwa bahati mbaya hatukuweza kuzitumia vizuri ikiwemo nafasi nne za wazi ambazo Morrison alizikosa.“

 

Lakini kwangu nilifurahishwa na viwango vya wachezaji wote kwani walijitahidi sana kupambana hasa kwa kuwa walicheza katika mazingira magumu kidogo na yale ambayo wameyazoea, lakini tayari kama benchi la ufundi tumefanya tathimini ya jumla ya mchezo huo na kuyarekebisha, hivyo naamini tutafanya vizuri.

STORI: SAID ALLY NA JOEL THOMAS


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad