Laini za Simu Kuwekwa ‘Password’ Kuanzia Julai Mosi




MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema ifikapo Julai mosi, laini zote zitakazotolewa zitakuwa na neno la siri ambalo mteja atatakiwa kulibadilisha ili kutumia laini mpya yenye usalama.


Kwa mujibu wa ujumbe uliosambazwa jana kwenye simu za wateja mbalimbali ambao ulithibitishwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa TCRA, Semu Mwakyanjala, utaratibu huo utalinda wateja.


Alisema utaratibu huo una lengo la kuwalinda wananchi kwenye matumizi ya mawasiliano.

“Laini inapopotea ikachukuliwa na mwingine anaitumia vibaya lakini kwa kuwa na neno la siri, itamlinda mtumiaji na kuondokana na utumiaji usio salama,”alisema.

Mwakyanjala alisema utaratibu huo ni kwa mujibu wa sheria ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010 na kanuni zake za 2018.


“Tunataka matumizi bora ya mifumo ya simu si kwa ajili ya kuongea bali kama benki, hivyo usalama ni muhimu kwa ajili ya kuwalinda watumiaji, watu watumie simu kwa biashara na maendeleo kuliko kufanya uhalifu,”alisema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad