Nyota wa filamu za Hollywood Lupita Nyong'o anatambulika kwa rangi yake ya ngozi, sauti tamu na kipaji cha uigiza.
Lupita Nyongo awadondosha 'mafisi' mate na kiuno chake cha nyuki akidensi
Lupita Nyong'o awadondosha 'mafisi' mate na kiuno chake cha nyuki akidensi.Picha:Lupita Nyong'o.
Lakini kuna sifa zingine kando na tabia zake ambazo wafuasi wake hawakuwa wanafahamu.
Lupita anaweza kusakata densi, si kucheza tu bali pia kunengua kiuno chake mithili ya nyuki na kumshinda mwanamke yeyote kutoka Jamaica.
Hivi majuzi kuliibuka wimbi la densi maarufu kama “Jorochallenge" ambayo wengi wamekuwa wakishiriki kupitia kurasa zao za Instagram ikiwemo muigizaji huyo.
Katika densi hiyo, wanawake wanaonyeshwa wakinengua viuno vyao wakiwa wamebeba vyombo kwenye vichwa vyao.
Lupita pia alijiunga na wimbi la densi hiyo ambapo aliwatumbuiza wengi wakati alikuwa ananengua kiuno chake akiwa amebeba tunda kichwani.
Aliwaduwaza wafuasi wake wa Instagram na kuwaacha kila mmoja aliyetazama video yake ameshangaa.
Kwa kweli inaridhisha moyo kumuona nguli huyo akiweka upya tabasamu kwenye uso wake baada ya kumpoteza rafiki wake wa karibu na pia muigizaji mwenza Chadwick Boseman.
Lupita, mnamo, Jumatano, Septemba 8, alijiunga na ulimwengu mzima kumuomboleza marehemu Boseman na ujumbe wa kuhuzunisha.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Lupita ambaye aliigiza kama Nakia katika filamu ya kampuni ya Marvel, alichapisha picha yake na Chadwick wakiwa wamejawa na furaha, na kisha kuiambatanisha na ujumbe mrefu wa kuzua kumbu kumbu yake na marehemu.
Lupita alisema ilikuwa vigumu kuamini kuwa Chadwick alifariki na ataishi kumkumbuka maisha yake yote kwa wema wake.