Mahakama yaridhia kuuzwa mali za Mmiliki wa Impala hotel





Mahakama kuu Kanda ya Arusha imeridhia kuuzwa kwa mali za Mmiliki wa hotel za Impala na Naura Spring ikiwemo viwanja vinne ili kufidia malipo ya Wafanyakazi 238 yanayofikia shilingi milioni 500.

Mahakama hiyo pia imeridhia maombi ya Benki ya Biashara ya NBC inayoidai hotel ya Impala shilingi Bilioni 1.5 ili fedha zitakazobaki baada ya Mali za mdaiwa kuuzwa na kulipwa Wafanyakazi zikabidhiwe kwa Benki hiyo na sio kwa mdaiwa.

Jaji wa Mahakama hiyo Mohamed Gwae amesema baada ya Mahakama kupitia pingamizi za Mmiliki wa hoteli hizo akipinga uamuzi wa Msajili wa Mahakama kuu Kanda ya Arusha, Masijala ndogo ya kazi juu ya kuuzwa kwa mali zake ili kufidia malipo ya Wafanyakazi, amesema ameona hayana mashiko.

Jaji Gwae ameamuru viwanja namba 20,21,22 na 23 vilivyopo block B Uzunguni, jijini Arusha kuuzwa na kufidia mishahara ya Wafanyakazi wapatao 238 wakiwemo 68 wa hotel ya Naura wanaodai zaidi ya milioni 107 na Wafanyakazi 167 wa hoteli ya Impala wanaodai milioni 397 huku magari na jenereta yanayoshikiliwa na Dalali wa Mahakama yaendelee kushikiliwa.

Awali upande wa waleta maombi ukiwakilishwa na Wakili Ngereka Miraji ulipinga Afisa kazi Mkoa wa Arusha kusimamia madai ya Wafanyakazi hao ukidai kwamba hana mamlaka kisheria ispokuwa Kamishna kazi pekee, madai ambayo yalitupwa na Jaji Gwae.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad