Rais Yoweri Museveni aliingia madarakani mwaka 1986Image caption: Rais Yoweri Museveni aliingia madarakani mwaka 1986
Marekani inastahili "kuangazia uchaguzi wake" badala ya "kuisomea" Uganda kuhusu uchaguzi wake, msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo amenukuliwa na gazeti la New Vision linalohusishwa na serikali.
Tamko lake linakuja baada ya Marekani kusema inatafakari "kuchukua hatua" baada ya uchaguzi wa Uganda kukumbwa na "ghasia" na "unyanyasaji" uliofanywa na vikosi vya usalama.
Akijibu hilo, Bw. Opondo alisema Uganda itasubiri mawasiliano rasmi kutoka kwa serikali ya Marekani.
"Kwa sasa, nadhani serikali ya Marekani inastahili kushughulikia uchaguzi wake, ambao kulingana na Rais Donald Trump, hata wapigakura waliokufa walishiriki uchaguzi wakati Joe Biden yuko madarakani kupitia njia ya udanganyifu.
Kwa hivyo wao wanastahili kuwa wa mwisho kutupatia somo,” Bw Ofwono alinukuliwa kusema.