Marekani inasema Mwanamfalme wa Saudia aliidhinisha mauaji ya Khashoggi




 Ripoti ya kijasusi ya Marekani imebaini kuwa Mwnamfalme wa Saudia Arabia Mohammed bin Salman aliidhinisha mauaji ya mwandishi wa habari wa nchi hiyo aliyekuwa ukimbizini Jamal mwaka 2018.



Ripoti iliyotolewa na utawala wa Bw Biden inasema mwanamfalme aliidhinisha mpango wa "kumkamata au kumuua" Khashoggi.



Marekani ilitangaza vikwazo kwa makumi kadhaa ya Wasaudia lakini sio dhidi ya mwanamfalme mwenyewe.



Saudi Arabia ilipinga ripoti hiyo ikiitaja kuwa "hasi, uongo na isiyokubalika ".





Mwanamfalme Mohammed, ambaye anatambuliwa kama mtawala wa ufalme, amekanusha kuhusika kwa namna yoyote ile katika mauaji hayo.


Khashoggi aliuawa alipokuwa akiutembelea ubalozi mdogo mjini Instanbul , Uturuki , na mwili wake ulikatwa katwa.



Mwandishi huyo wa habari aliyekuwa na umri wa miaka 59 wakati mmoja aliwahi kuwa mshauri wa serikali ya Saudi Arabia na alikuwa karibu sana na utawala wa Ufalme , lakini alikosana nao na kwenda nchini Marekani mwaka 2017.



Akiwa nchini Marekani, aliandika waraka wa kila mwezi katika gazeti la Washington Post ambapo alikosoa sera za Mwanamfalme Prince Mohammed.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad