Mastaa 8 Simba SC Kuwakosa Waarabu




DIDIER Gomes huenda akawakosa nyota wake nane kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Februari 23.

 

Nyota hao ambao kwa ujumla wamehusika kwenye mabao 12 kwenye Ligi Kuu Bara kati ya 42 yaliyofungwa na Simba, watakosekana kikosi cha kwanza kutokana na sababu mbalimbali ambazo zinawakabili.

 

Mshambuliaji mzawa namba moja, John Bocco ambaye ana mabao 8 na pasi mbili za mabao, bado hajawa fiti huku Perfect Chikwende ingizo jipya ndani ya Simba, kutoka FC Platinum akiwa ametoa pasi ya bao moja mbele ya Dodoma Jiji hayupo kwenye mpango wa mechi za kimataifa.



Nyota sita wa kikosi cha Simba waliachwa Congo na timu ilipokwenda kuwatungua bao 1-0 AS Vita kutokana na kile ambacho kimeelezwa kuwa mamlaka ya Congo iliwataka wabaki huko kwa uangalizi maalumu kwa madai kwamba wana Virusi vya Corona na jana walirejea Bongo.

 

Kipa namba tatu, Ally Salim, Kennedy Juma, Ibrahim Ame,Erasto Nyoni ni mabeki, kiungo Larry Bwalya ana asisti 1 mbele ya JKT Tanzania na kiungo mkabaji Jonas Mkude.

 

Pia yupo meneja wa Simba, Abas Seleman. Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alikiri kuwa wachezaji sita wa timu hiyo walibaki nchini DR Congo kutokana na kile ambacho mamlaka ya nchini humo kudai kuwa wana maambukizi ya Corona licha ya Bwalya na Kened kucheza mchezo huo.

 

“Wachezaji pamoja na meneja (Abas) wameingia leo (jana) kutoka DR Congo na moja kwa moja wameingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly ya Misri hivyo wanaongeza upana wa uteuzi wa kikosi kitakachoanza kwenye mchezo wetu.”


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad