Mbunge akumbusha kilio cha Katiba Mpya

 



Dodoma. Mbunge wa viti maalum, Kunti Majala amesema bila Katiba mpya faraja ya wapinzani nchini Tanzania ni ndoto.


Kunti ni miongoni mwa wanawake 19 waliovuliwa uanachama wa Chadema wakidaiwa kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama hicho.


Hata hivyo, wote wanahudhuria vikao vya Bunge la 12 linaloendelea mjini Dodoma huku wakiwa wamekata rufaa kupinga kamati kuu ya Chadema  kuwavua uanachama.


Akizungumza bungeni leo Alhamisi Februari 4, 2021 katika mjadala wa hotuba ya Rais John Magufuli ya uzinduzi wa Bunge la 12, Kunti amesema, “tunaomba Katiba mpya, tunasisitiza kupatiwa Katiba mpya ambayo tunaamini itatupatia tume huru ambayo ni faraja kwa wapinzani.”


Kunti ambaye aligombea ubunge Chemba katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2020, amesema wapinzani wana maumivu makali yaliyotokana na uchaguzi na kusisitiza kuwa Katiba wanayoitaka ni yenye maoni ya wananchi itakayotoa dira na maelekezo ya kuundwa tume huru ya uchaguzi.

 

  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Bila kutaja yaliyompata katika uchaguzi huo, amesema kitanda ambacho mtu hajakilalia hawezi kujua kunguni waliomo, “lakini waliokilalia wanajua ukweli.”


Kwa mujibu wa Kunti,  hata uchaguzi ukiitishwa sasa bado kutakuwa na kilio cha wapinzani na kwamba Katiba mpya ndio suluhisho la kilio hicho

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad