Meli ya mizigo ya kibiashara iligongana na manowari ya Kikosi cha Wanamaji wa Japan (MSDF) katika pwani ya mkoa wa Kochi nchini Japan.
Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa 10.50 za asubuhi kwa saa za ndani, kwenye maeneo ya mbali na ufukwe wa Asizuri ulioko pwani ya Kochi ya Pacific.
Kulingana na shirika la Kyodo, inakadiriwa kuwa wahudumu 3 wa MSDF walijeruhiwa baada ya mgongano huo.
Hakuna uharibifu ulioripotiwa kwenye manowari hiyo baada ya mgongano.
Mawasiliano yalianzishwa na Kituo cha Usimamizi wa Mgogoro cha Ofisi ya Waziri Mkuu (Kantei) kuhusiana na tukio hilo.