Mijusi wawili ilibainika nchini Madagasca na timu ya sayanasi ya Ujerumani na Madagasca.
Mjusi wa kiume aliyepewa jina la Brookesia urefu wake ni milimita 13.5.
Na mjusi huyo anakuwa mdogo zaidi kati ya spishi karibu 11,500 za mijusi, kulingana na rekodi ya hifadhi ya wanyama ya taifa ya Bavaria katika mjini mkuu wa Munich.
Urefu wake kutoka juu hadi chini ni milimita 22.
Mjusi wa kike ni mkubwa kidogo takribani milimita 29, taasisi hiyo imesema, ikiongeza kwamba aina nyingine bado hazijapatikana, licha ya kwamba "juhudi zimekuwa zikiendelea".
"Mjusi huyo mpya aliyepatikana kaskazini mwa Madagascar eneo la msitu linalopokea mvua kubwa, huenda yuko katika hatari ya kutoweka," kulingana na jarida la wanasayansi.
Oliver Hawlitschek, mwanasayansi wa kituo historia huko Hamburg, alisema: "Kwa bahati mbaya eneo alilokuwa akiishi mjusi huyo lilianza kuingiliwa na binadamu lakini likaanza kulindwa hivi karibuni, kwahiyo anawezaa kunusurika."
Watafiti walibaini kwamba mjusi huyo alikuwa anatafuta mchwa katika msitu wenye mvua kubwa na kujificha dhidi ya wanyama wala nyama usiku kwenye nyasi.
Katika msitu ambao mjusi Brookesia alipatikana umepakana na misitu mingine kaskazini mwa kisiwa, walisema.
Katika ripoti yao, wanasayansi wamependekeza kuwa mjusi huyo aorodheshwe kama mnyama aliye hatarini katika orodha ya Shirika la IUCN, linalochunguza hali ya maelfu ya jamii za wanyama kumsaidia kumlinda na makazi yake.