Mke wa El Chapo Emma Coronel Aispuro akamatwa Marekani kwa 'Ulanguzi wa mihadarati'




Mke wa mlanguzi mkuu wa mihadarati kutoka Mexico El Chapo Guzman amekamatwa nchini Marekani kwa tuhuma za ulanguzi wa mihadarati , imesema mamlaka nchini humo.
Emma Coronel Aispuro , mwenye umri wa miaka 31 alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles nje ya mji mkuu wa Washington DC.

Anashtakiwa kwa kushiriki katika njama ya kutaka kusambaza dawa aina ya Cocaine, Methamphetamine, heroin na bangi.

Guzman kwasasa anahudumia kifungo cha maisha jela mjini New York kwa kuhusika katika ulanguzi wa mihadarati na fedha.

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 63 ni kiongozi wa zamani wa kundi la walanguzi wa mihadarati wa Sinaloa ambalo ndilo lililokuwa na mtandao mkubwa wa usambazaji wa mihadatari nchini Marekani.

Kesi yake mwaka 2019 iligundua mambo ya kushangaza kuhusu maisha yake , kutoka kuwapatia wasichana mihadarati na kuwabaka wakati alipokuwa na umri mdogo wa miaka 13 mbali na kuwaua baadhi ya wanachama wa genge hilo na wapinzani.

Bi Coronel Aispuro anatarajiwa kuwasilishwa mbele ya mahakama ya kijimbo mjini DC kupitia kanda ya video , imesema idara ya haki nchini humo.

Mbali na kukabiliwa na mashtaka ya ulanguzi wa mihadarati , pia anatuhumiwa kushirikiana na wengine kumsaidia mume wake kutoroka jela nchini Mexico 2015.

Alitoroshwa katika jela ya Altiplano nchini Mexico baada ya wanawe kununua jumba lililokuwa karibu na jela hiyo na kuingiza aina ya saa ya GPS ndani ambayo iliwaonesha wachimbaji jela ambayo el Chapo alikuwa anazuiliwa.

Alitoroka kwa kutumia pikipiki ndogo ndani ya handaki hilo.

Stakhabadhi za mahakama zilisema kwamba bi Coronel Aispuro alidaiwa kuhusika katika kupanga kumtorosha mume wake katika jela nyengine kabla ya kufurushwa nchini Marekani mwezi Januari 2017.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad