Mkuu wa Olympiki ya Tokyo ajiuzulu na kuomba radhi






Mkuu wa michezo ya Olympiki ya Tokyo mwaka 2020 Yoshiro Mori amejiuzulu Ijumaa na kuomba msamaha tena kwa matamshi yake ya kashfa ya kijinsia ambayo yalisababisha lawama ulimwenguni.


Kiongozi huyo amejiuzulu wakati kamati ya Olimpiki ikiwa kwenye shida ya kutafuta kiongozi mkuu miezi mitano kabla ya michezo hiyo kuanza.



"Maoni yangu yasiyofaa yalisababisha shida kubwa. Samahani," Mori, mwenye umri wa miaka 83, alisema katika mkutano wa kamati ya maandalizi ya Olympiki.



Alisema jambo la muhimu zaidi sasa ni kwamba Olympiki ya Tokyo iweze kufanikiwa.



Kujiuzulu kwake kukiwa ni miezi michache kabla ya Michezo ya Majira ya joto ya Olimpiki kufanyika kutaharibu zaidi imani kwa uwezo wa waandaaji kufanikisha hafla hiyo, wakati wa janga la virusi vya corona. Michezo awali ilipangwa kufanyika mwaka jana.



Mori, Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, alizua hasira wakati aliposema kwenye mkutano wa kamati ya Olimpiki mapema mwezi Februari kwamba wanawake wanaongea sana.



Baada ya kilio ulimwenguni kwamba aondolewe aliomba msamaha kwa maoni yake lakini alikataa kuachia ngazi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad