Morocco Mabingwa Tena CHAN

 


Timu ya Taifa  ya Morocco usiku wa jana tarehe 7/2/2021 waliibuka mabingwa wa michuano ya CHAN  baada ya kuifunga Mali 2-0 kwenye mchezo wa fainali  uliochezwa uwanja Ahmadou Ahidjo katika mji wa Yaounde, huku Mali akishika nafasi ya 2 na Guinea nafasi ya 3 na Cameroon ya 4

Morocco wamefanikiwa kutetea ubingwa wao, walioutwaa mwaka 2018 katika ardhi ya nyumbani kwao, huku ikitumia wachezaji wengi waliokuwepo katika mafanikio yaliyopita, akiwemo Ayub el Kaab ambaye aliibuka mfungaji bora wa michuano hiyo


Ubingwa wa Morocco ulitarajiwa na wengi kutoka na ubora wa timu yao hasa ukizingatia wachezaji wake wengi wanacheza katika  vilabu vya ndani vikubwa kama Raja Casablanca, Wydad Casablanca na RS Berkane ambavyo vinavyofanya vizuri katika michuano mikubwa ya Africa, kama vile klabu bingwa na kombe la shirikisho la CAF.


Morocco pamoja na kutwaa kombe la mashindano hayo, pia ilizoa  tuzo nyingine kama, ile ya mfungaji bora, na mchezaji bora wa mashindano ambayo imeenda kwa Soufiane Rihimi, pia tuzo ya golikipa bora imekwenda  kwa kipa wao Anas Zniti.


Michuano hiyo iliyoanza tarehe 16/1/2021 na kumalizika tarehe 7/2/2021 imeshuhudia magoli 62 yakifungwa katika michezo 32 iliyocheza, ikiwa ni wastani wa goli 1.94 kwa mechi, Mmoroco Soufiane Rihimi ameibuka mfungaji bora kwa mabao 5, Mali imetwaa tuzo ya timu yenye nidhamu bora katika mashindano hayo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad