Mrisho Gambo: “Sijaridhika na Majibu” Spika Amtuliza




Spika wa Bunge Job Ndugai, amefurahishwa na swali lililoulizwa na mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo, kwamba Wizara ya Maliasili haioni umuhimu wa kusitisha tozo kwa hifadhi zilizochini ya TANAPA ambao tozo zake ziliongezwa ili kutoa fursa ya ya sekta ya utalii ambayo imethirika na Corona.

 

 

Hayo yamejiri hii leo Februari 8, 2021, Bungeni Dodoma wakati wa kikao cha Tano, mkutano wa PIli wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo kupitia hoja hiyo pia Spika Ndugai alimshi mbunge Gambo kuongeza hoja zake na nafasi bado anayo kwani haiwezekani idadi ya watalii ipungue halafu tozo zibaki kuwa zile zile.

 

 

“Sekta ya utalii kwa mkoa wa Arusha na nchi nzima imeathirika sana wananchi wengi wamekosa ajira, madereva wamekosa ajira kwa sababu magari hayatembei kutokana na uchahche wa ajira, tukiangalia kwenye ukanda wa Afrika Mashariki nchi nyingi zimepunguza tozo.

 

“Je Wizara ina mpango gani wa kuipa ahueni sekta ya utalii ili kuweza kunusuru changamoto kubwa ya ajira”, amesema Mrisho Gambo.

 

 

Akichangia katika hoja hiyo Spika Ndugai ameongeza kuwa, “Swahi hili lina msingi sana, Mh. Gambo bado una nafasi tunaelekea kwenye mipango na bajeti unaweza ukafafanua zaidi hoja yako, ni hoja yenye mvuto na ya msingi sababu haiwezekani graph ya watalii inapungua halafu wewe unaongeza bei”.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Gambo, hoja yako ina Mashiko. Duniani baada ya mlipuko wa kolona kila sekta na wizara zinapeleka mapendekezo serikali kuu vipi wafanye stimulus options ili mwananchi asiathirike zaidi. na sisi sio mpaka tungoje mtetezi wetu JPM Alitolee kauli.

    Kwa sasa pia TRA pia waangalie na kuondoa kodi kwa Watanzania wengi wanao rudi nyumbani na familia zao baada ya kupoteza Ajira Ughaibuni. waweke utaratibu kwa huyu mtanzania anaaehamisha makazi na si kumuongezea machungu na pia wapewe kipa umbele kaatika kujiunga na Elimu za juu na mikopo stahiki.

    Wabunge amkeeni katika kutuemea changamoto zetu, Msukuma, Gambo. Well Done

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad