Mimi ni kijana, miaka 27. Ninaishi na kufanya kazi mkoani nyanda za juu kusini huku. Nina kazi nzuri na vibiashara vya hapa na pale vya kuniweka mjini. Nilikua na malengo mengi sana na swala la kuoa sikua nimelipanga kwa sasa. Sikua na uhusiano wowote serious.
Mwaka jana mwanzoni kuna binti nilikutana nae maeneo ya mjini, ni mzuri sana na ana kazi yake nzuri tu, very social na ana roho nzuri sana tulibadilishana contacts baadae tukaanza kuwasiliana na baada ya kama wiki tukafanya mapenzi.
Alionesha kunipenda toka tunakutana. Akataka tuendelee na uhusiano, nikamwambia sawa lakini nikamfahamisha kuwa mimi sina mpango wa kuoa hivi karibuni so kama ana mtafuta mwanaume wa maisha yake sio mimi kwa sasa.
Alilia sana siku ile nikajua tumeshaachana. Lakini baadae akanitafuta na kuniambia hana shida tuendelee.
Tukapima na kuendelea na uhusiano. Mara ya kwanza tulitumia kinga. Nkaona ili twende sawa, nijue mzunguko wake wa mwezi na lini yupo safe na lini yupo danger.
Baada ya miezi miwili akaniambia ana mimba ya wiki 3. Nikivuta picha katika hyo wiki ya kutunga mimba nilionana nae mara moja tu, nlikua busy sana na mdogo wangu alikua amekuja kwangu kipindi hicho, hyo siku alilazimisha sana tuonane na kunihakikishia kuwa yupo safe mpaka ikabidi twende lodge. Kwake alikua anaishi na binamu yake
Nkapata picha either mimba sio yangu au kanitegeshea. Nkamuita nkakaa nae chini na kuongea nae kwa kirefu sana. Nkamuambia kama mtoto sio wangu ntajua tu na hakuna kitakachoendelea kati yetu. Na hata kama ni wangu, siwezi kubadilisha plan zangu za maisha so asiwaze kabisa kama ataolewa coz amebeba mimba. Alichoniambia ni kuwa mimba ni yangu na anaomba walau shangazi yake aliekua anaishi huku mkoani anifahamu ili tumbo likitokeza atleast kuwe na idea ya aliempa mimba. ( kwa huyu shangaz yake ndo alikokua anaishi alipokuja kuripoti kazini kabla ya kupanga na binti wa huyo shangazi). Nkamuambia sawa lakini sijawahi kwenda huko wala kwao mpaka leo.
Nilifanya uchunguzi wangu mkali lakini sikuona kama kuna dalili yoyote kama mimba si yangu. Nkaona mtoto akizaliwa tutajua. Ilivofika miezi saba nilimshirikisha mama. Mama akasema anataka amuone. Nkamuomba mama aje na kweli alikuja na akaonana nae. Alipojifungua alienda kwao na gharama zote mimi ndo nlihusika na mpaka sasa nahusika. Baada ya kumaliza uzazi wazee wangu hasa baba wakataka wamuone yeye na mtoto, uzuri wote ni wastaafu so walikuja wakamuona. Tunaishi mkoa mmoja wilaya tofauti so wanakuja na kuondoka siku hyo hyo.
Huyu binti alivoona wazee wangu ni wastaafu na sisi watoto wote tuna kazi zetu na tupo busy sana na maisha akajiweka karibu nao. Weekends anaenda kushinda huko full kuwapikia na kuwafanyia mambo mengi. Mimi nilikua sijui coz siishi nae na huwa niko busy sana. Ratiba yangu ya kuonana na wazee ni mara moja kwa mwezi au sometimes kwa miezi miwili naenda mara moja. Changamoto ni kuwa wazee wamemuelewa sana na wananilazimisha niishi nae, na yeye kakomaa muda wote analia anataka aje tuanze maisha, home kwao nao wamechachamaa wanataka nikajitambulishe na nitoe posa.
I feel conerned, coz haya mambo hayakuwa plani yangu na najua huyu binti kanitegeshea mimba makusudi ili aolewe na ana wanipulate wazee wangu ili wawe upande wake. Mtoto najua ni wangu coz tunafanana sana, kachukua kila kitu kwangu. Nawaza sana kuhusu hili swala mpaka nmeanza ku apply kazi nje ya huu mkoa nikaanze upya.
I wish nipate mawazo tofauti labda ntajua cha kufanya.