Msajili wa vyama awaonya upinzani mbele ya Rais

 


Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amemuagiza Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, kwamba akawaambie wapinzani wenzake watulie na waache kuwasilisha masuala ya Bunge kukiwa na masuala ya Kitaifa na kwamba huu mwaka 2021 wawe na uzalendo.

 


Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari Mosi, 2021, wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria na miaka 100 ya Mahakama ya Tanzania, mara tu baada ya Profesa Ibrahimu Lipumba kuzungumza na kumuomba Rais Dkt. Magufuli, kutimiza ahadi zake alizozitoa kuhusu upatikanaji wa katiba mpya.


"Mimi kama msajili wa vyama vya siasa bila kigugumizi chochote ninaweza nikasema hata vyama vya siasa vimekuwa na imani kubwa na Mahakama zetu, ndiyo maana kila nikitoa maamuzi wanakimbilia Mahakama, ninachowaomba muendelee kuiamini", amesema Jaji Mutungi


"Ndugu yangu Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Mh. Rais nimesikia anakuomba kuhusiana na katiba nilijua lazima wanasiasa watakukumbushia, namuomba Profesa Lipumba akawaambie wenzake ule mchezo wa kutoka toka kwenye mabunge kukwamisha haya masuala muhimu ya kitaifa basi wayapunguze, 2021 tuwe ni watu wenye uzalendo tukiwa na masuala ya kitaifa mambo ya kuinuka inuka kutoka kwenye Bunge hayo tuyaache", amesema Jaji Mutungi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad