Msumbiji:Eneo la kuhifadhia maiti kuongezwa baada ya ongezeko la vifo vilivyotokana na corona





Msumbiji imerekodi vifo 210 kutokana na corona kuanzia Januari, ambao ulikua mwezi mbaya tangu kuanza kwa jangaImage caption: Msumbiji imerekodi vifo 210 kutokana na corona kuanzia Januari, ambao ulikua mwezi mbaya tangu kuanza kwa janga
Maafisa wa mji wa Msumbiji wa Chimoio wametangaza mipango ya kuongeza chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali kuu ya jimbo kutokana kuongezeka kwa idadi ya vifo vinavyotokana na Covid-19.

João Ferreira, Meya wa jiji amethibitisha kuongezwa kwa eneo la chumba hicho.

Mradi huo utajumuisha kuongezwa kwa jengo la kuhifadhia maiti na kuongeza uwezo wa jokofu za kuhifadhia maiti kwa gharama ya thamani ya dola 5,300 (£3,800) katika hospitali ya jimbo la Manica Chimoio.

Chumba cha kuhifadhia maiti ambacho kinaendeshwa na halmashauri hivi karibuni kiliongezewa uwezo kuanzia miili mitano hadi 60.

Jiji limekuwa na wastani wa vifo vitano kila siku.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad