Fahamu taarifa za awali za msiba wa Mambo
JUMATATU , 8TH FEB , 2021
NA MWANDISHI WETU
Mwandishi wa habari Mukhsin Mambo, amefariki dunia hii leo Februari 8, 2021, akiwa nyumbani kwake nchini Marekani. Mambo, amewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital hii leo Februari 8, 2021, Bernard James, ambaye ni mmoja wa watu aliowahi kufanyanao kazi amesema kuwa taratibu za msiba zinafanyika jijini Mwanza maeneo ya Capripoint kwa Dada yake.
Aidha James ameongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa za awali zinadai Mambo, alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa kipindi cha muda mfupi na kwamba mpaka mauti yanamfika alikuwa anajisikia vibaya kabla ya kukimbizwa hospitali.
Mukhsin Mambo amewahi kufanya kazi katika kituo cha Radio Free Africa (RFA) Mwanza na TV1.