Muimbaji staa Diamond atua Nairobi na jeti ya kifalme








Mashabiki Wakenya wa msanii nyota wa Bongo Diamond Platnumz walikuwa na furaha kumuona mwanamuziki huyo nchini.


 
Baba lao Diamond atua Nairobi na jeti ya kifalme
Diamond wakati wa mahojiano na Wasafi.Picha:diamondplatnumz.
Muimbaji huyo maarufu atatumikia siku yake ya Jumapili, Februari 7, nchini Kenya lakini bado haijabainika wazi ziara yake ni ya siku ngapi.

Hii ni baada ya Diamond kuchapisha video akiwa ndani ya jeti hiyo ya kifahari na kuvalia mavazi yenye rangi ya manjano na nyeusi.


Katika video hiyo, Diamond anaonyeshwa akiabiri jeti akiwa amebeba begi ya pesa kawaida na mwenendo wake na kisha kupiga tama soda aliyokuwa amebeba.

Video hiyo pia inaonyesha sehemu ya ndani ya jeti hiyo ambayo ilikuwa imeabiriwa na Diamond pekee.



Bado haijabainika wazi misheni ya muimbaji huyo nchini Kenya lakini kutokana na kuanika kampuni ya soda aliyokuwa akinywa, inaonyesha kuwa ni mambo ya kibiashara bali si tamasha kama wengi walivyokuwa wanatarajia.

Pia haijathibitishwa wazi endapo atatenga muda wa kuwa na mama wa mtoto wake Naseeb jr.

Haya yanajiri siku chache baada ya Tanasha kupiga ziara nchini Tanzania na kuibua fununu kuwa wapenzi hao wa zamani wamerudiana.

Waliwatumbuiza mashabiki pamoja kwenye jukwaa na kuzua hisia mseto kutoka kwa mashabiki kulingana na namna wawili hao walikuwa wakisakata densi pamoja.

Hata hivyo, walizungumzia kuhusu uhusiano wao na kuweka wazi kuwa hawatarudiana.

Tanasha pia alitaja sababu ya busu lake kuonekana kukataliwa na Diamond wakiwa jukwaani, akidai alikuwa anataka tu kumnongonezea jambo.


 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad