KOCHA Mkuu wa Klabu ya Namungo, Hemed Morocco amesema kuwa mambo ambayo wamekutana nayo nchini Angola ni sehemu ya mchezo jambo ambalo linawafanya wajipange kwa ajili ya wakati ujao.
Namungo Februari 12 ilisafiri kutoka Bongo mpaka Angola kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora dhidi ya 1 de Agosto ya Angola.
Kilizuiwa Uwanja wa Ndenge wa Luanda Februari 13 kwa kile ambacho kilielezwa kuwa wachezaji wao watatu pamoja na kiongozi mmoja kukutwa na Virusi vya Corona.
Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) pamoja na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya nje waliweka nguvu kwenye kufuatilia suala hilo ambapo majibu yalitolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwamba mchezo wao ambao ulipaswa kuchezwa leo umefutwa na Kamati ya maadili italifuatilia suala hilo kwa ukaribu.
Akizungumza na Saleh Jembe, Morocco amesema kuwa wanashukuru Mungu wapo salama ila yaliyotokea ni somo kwao.
"Ni changamoto kwetu na ni somo pia hivyo hatuna la kusema kwa sasa,tunarejea kujipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo" ..