“ Ukusanyaji wa kodi ni taaluma ya muda mrefu sana lakini changamoto tulionayo ni kwamba tumeamua kuacha kuwatumia wataalamu ambao ndio wakusanya kodi.“
“Sasa kinachotokea wanakwenda kwa mfanyabiashara hawajali maisha yake ya kesho hawajali kwamba wanatakiwa kukusanya kodi leo hawamuachii uwezo wa kuzalisha ili wakusanye na kesho, sasa tunafurahia matokeo ya muda mfupi kwa sababu idadi ya biashara zinazofungwa ni nyingi mno kesho hatuna ng’ombe wa kumkamua maziwa,” amesema mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye.