Kombe la Dunia kwa vilabu bingwa wa mabara yanaanza leo tarehe 4/02/2021 hadi 11/02/2021 nchini Qatar, katika viwanja vitatu tofauti Ahmad bin Ali, Education City na Khalifa International.
Michuano hii, hukutanisha mabingwa wa mashirikisho ya mabara yote 7, kama UEFA, CAF CONMEBOL ,AFC, CONCACAF na OFC ambapo Africa tunawakilishwa na Al Ahly ya Misri.
Fungua dimba itahusisha mechi mbili, Tigres UANL dhidi ya Ulsan Hyundai na ile ya pili itakuwa AL Duhail na Al Ahly ambao ndio wawakilishi kutoka bara la Africa wakiwa na uzoefu mkubwa wa kushiriki mashindano hayo.
Katika timu ya Al Duhail yupo mchezaji Michael Olunga raia wa Kenya anayecheza soka la kulipwa huko,ambapo mshindi wa mechi hii atakutana na mabingwa wa Ulaya kutoka shirikisho la UEFA ambao ni Bayern Munich.
Bayern Munich wanatarajiwa kuwa mabingwa kama ilivyo desturi ya washindi kutoka katika shirikisho la UEFA, ambaye hadi sasa bingwa mtetezi ni Liverpool, huku Real Madrid akiongoza kwa kutwaa ubingwa mara 4, Barcelona 3.
Munich wanaonekana kuyapa mashindano haya kipaumbele cha hali ya juu kwa kuorodhesha wachezaji wake bora kama Thomas Muller, Manuel Neuer na Robert Lewandowski miongoni wa majina 23 yanayotakiwa.