Polisi waliosababisha kifo cha raia mwenye asili ya Kiafrika Daniel Prude, ambaye alizuiliwa uchi katika Jiji la New York, Marekani karibu mwaka mmoja uliopita na kuwekea mfuko wa plastiki kichwani mwake, wameonekana kutokuwa na hatia.
Katika taarifa iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu wa New York, iliarifiwa kwamba maafisa wa polisi ambao walisababisha kiwewe na kifo wiki moja baadaye kwa sababu ya mfuko wa plastiki walioweka kichwani mwa Prude mwenye ulemavu wa akili, hawatoweza kuhukumiwa baada ya jopo kuu la majaji kukataa mashtaka hayo.
Wakili Mkuu Letitia James, ambaye alifanya uchunguzi, alisema kuwa faili walilotayarisha "lilikuwa na ushahidi wenye nguvu zaidi" lakini hawakuweza kushawishi jopo kuu kwamba maafisa hao walifanya uhalifu.
James alisema, "Natambua kwamba familia ya Prude, jamii ya Rochester pamoja na watu wengi kote nchini wangekatishwa tamaa na matokeo haya."
Elliot Shields, wakili wa familia ya Prude pia alisema, "Mfumo huu ulifanya makosa tena juu ya Daniel Prude. Ilikuwa ni makosa kuruhusiwa kutoka hospitalini mnamo Machi 22. Polisi walikosea kutumia nguvu iliyosababisha kifo chake mnamo Machi 23, na leo hii wameachwa bila hukumu."
Mamia ya waandamanaji walikusanyika katika jiji la Rochester, ambapo tukio hilo lilifanyika na kupinga uamuzi huo.
Video ya tukio hilo, ambayo lilifanyika mnamo Machi 23, 2020, ilisubiriwa kwa muda mrefu kutokana na maandamano ya George Floyd, mwenye asili ya Kiafrika, ambaye alikufa kutokana na kosa lingine la polisi, na video kuibuka mnamo Septemba 2020. Baada ya video hiyo, mkuu wa polisi wa Rochester alilazimika kujiuzulu.