Idara ya uhamiaji mkoa wa Kigoma imewakamata raia wa kigeni 52 kutoka nchi ya Burundi na jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo walioingia nchini kwa kutumia njia za panya wakiwemo wakimbizi 12 waliotoroka katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilaya ya Kasulu.
Akielezea kukamatwa kwa raia hao wa kigeni jana kaimu afisa uhamiaji mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi wa uhamiaji Augustino Matheo amesema raia hao wamekamatwa baada ya msako uliofanyika February 05 na 06 katika maeneo mbalimbali mkoani Kigoma uliofanikisha kukamata raia 43 kutoka nchi ya Burundi kati ya wakiwemo wakimbizi 3 na raia 9 kutoka nchi ya kidemokrasia ya Kongo ambao ni wakimbizi kutoka kambi ya Nyarugusu.
Pia Matheo ameeleza kuna watanzania watatu waliokuwa wakiwatumikisha raia hao nao wamekamatwa na baadae watafikisha mahakamani pamoja na wahamiaji hao .