Jeshi la Marekani limetekeleza shambulio la angani lililolenga wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran nchini Syria, Pentagon imesema.
Shambulio hilo liliharibu vifaa kadhaa vilivyokuwepo katika kituo cha mpakani kilichokuwa kikitumiwa na baadhi ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran, ilisema.
Rais Joe Biden aliidhinisha hatua hiyo ili kujibu mashambulio ya hivi karibuni dhidi ya maafisa wa Marekani na wale wa majeshi ya muungano unoaungwa mkono na taifa hilo nchini Iraq.
Mwanakandarasi mmoja aliuawa katika shambulio la roketi dhidi ya ya shambulio lililolenga maeneo ya Marekani nchini Iran mapema mwezi huu.
Afisa mmoja wa jeshi la Marekani na wanakandarasi watano walijeruhiwa wakati roketi hiyo iliposhambulia maeneo katika mji wa Irbil , ikiwemo kambi moja inayotumika na muungano wa majeshi yanayoungwa mkono na Marekani.
Mashambulio ya roketi pia yamepiga kambi za wanajeshi wa Marekani na maeneo ya wajumbe wa kidiplomasia.
Pentagon ilitaja Kataib Hezbollah na Kataib Sayyid al-Shuhada kama makundi mawili yanayoungwa mkono na Iran ilioyalenga katika shambulio la Alhamisi eneo la mashariki mwa Syria.
Ilitaja mashambuliko hayo kama jibu la kijeshi ambalo lilitekelezwa pamoja na hatua za kidiplomasia, ikiwemo kuwashauri washirika wake wa muungano wa majeshi.
''Operesheni hiyo imetuma ujumbe ulio wazi'' , ilisema taarifa ya Pentagon.
''Wakati huohuo , tumechukua hatua ya makusudi inayolenga kutochochea hali mbaya katika maeneo ya mashariki mwa Syria na Iraq''.