Rais wa Haiti adai kuwepo na njama za kumuua na kupindua serikali yake

 


Rais wa Haiti Jovenel Moise ametangaza jana kuwa polisi wamewakamata zaidi ya watu 20, wanaoshukiwa kupanga njama za kumuua na kuipindua serikali yake. 

Miongoni mwa waliokamatwa yumo Mkuu wa jeshi la polisi na jaji aliyekuwa akiungwa mkono na viongozi wa upinzani wanaotaka kiongozi huyo kuachia madaraka. 


Rais Moise amesema njama ya kumpindua ilianza Novemba 20 ingawa hakutoa maelezo zaidi. Upinzani umekuwa ukimshinikiza rais huyo kujiuzulu, ukidai kuwa muhula wake unamalizika Jumapili.


 Hata hivyo kiongozi huyo anadai kuwa muhula wake wa miaka mitano madarakani unamalizika Februari mwaka 2022. 


Upinzani uliandaa maandamano hivi karibuni ya kumshinikiza Moise kuachia madaraka. Anapanga kura ya maoni ya katiba mnamo mwezi Aprili ambayo wakosoaji wanasema inaweza kumpa nguvu zaidi, wakati uchaguzi mkuu umepangwa baadaye mwaka huu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad