Rekodi Zaibeba Yanga SC Dar leo

 



JESHI la Mrundi Cedric Kaze leo linatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kuvaana na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.


Yanga yenye pointi 45, itashuka uwanjani saa moja kamili usiku ikiwa na rekodi ya kupata matokeo mazuri ya nyumbani ya kushinda michezo tisa kati ya kumi waliyocheza ndani ya misimu kumi iliyopita dhidi ya Kagera na waliopoteza ulichezwa 2019/2020 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar ambao ulimalizika kwa Yanga kufungwa mabao 3-0.

 

Mingine yote walishinda ambayo ni Yanga 0:3 Kagera Sugar (2019/2020), Yanga 3:2 Kagera Sugar (2018/2019), Yanga 3:0 Kagera Sugar (2017/2018), Yanga 2:1 Kagera Sugar (2016/2017), Yanga 3:1 Kagera Sugar (2015/2016), Yanga 2:1 Kagera Sugar (2014/2015).


 

Nyingine ni Yanga 2:1 Kagera Sugar (2013/2014), Yanga 1:0 Kagera Sugar (2012/2013), Yanga 1:0 Kagera Sugar (2011/2012) na Yanga 2:0 Kagera Sugar (2010/2011).

 

Akizungumzia mchezo huo, Kaze alisema kuwa maandalizi ya pambano hilo yamekamilika kwa asilimia mia, kikubwa ataingia uwanjani kwa len-go la kupata pointi tatu ambacho ndio kitu cha umuhimu ili kuwapa furaha mashabiki.

 

“Ninafahamu umuhimu wa kila mchezo na hivi sasa ninauchukulia kila mchezo kama fainali kwa lengo la kuwaacha wapinzani kwa idadi kubwa ya pointi.“

 

Katika kuelekea mchezo huo, kikosi changu kitamkosa Saido (Ntibazonkiza), Yacouba (Songne) na Job (Dickson) wenye majeraha ambao wameanza mazoezi mepesi ya binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti.

 

“Kikubwa niwaahidi mashabiki kupambana kwa dakika 90 ili kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huu wa ligi dhidi ya Kagera,” alisema Kaze.Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, alisema kuwa: “Maandalizi ya kikosi changu yamekamilika na vijana wangu wapo fiti na morali ya kupata ushindi.”

GPL

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad