Rihanna azua balaa India, serikali yamshutumu, internet yakatwa Delhi



India imeshutumu ”raia wa kigeni” na watu maarufu kwa ujumbe waliotoa mtandaoni baada ya mwanamuziki Rihanna, kutangaza kuwaunga mkono wakulima wanaoandamana, hali iliyosababisha suala hilo kutolewa macho na jumuia ya kimataifa.


Saa chache baada ya ujumbe wa twitter wa muimbaji, mwanaharakati wa hali ya hewa Greta Thunberg, mpwa wa Makamu wa Rais wa Marekani Meena Harris pia aliandika kwenye ukurasa wa twitter kuwaunga mkono wakulima.


Ujumbe wao ulisambaa mtandaoni, ukijibiwa na maelfu ya watu.


Wakulima wamekuwa wakiandamana kwenye mipaka ya mji wa Delhi dhidi ya sheria mpya za kilimo.


Katika taarifa Jumatano, wizara ya masuala ya kigeni ya India ilisema bunge limepitisha “sheria ya mageuzi inayohusiana na sekta ya kilimo” baada ya majadiliano.


“Hashtags za kwenye mitandao ya kijamii na maoni, haswa yanapotolewa na watu mashuhuri na wengine, sio sahihi wala sio jukumu kwao,” iliongeza taarifa hiyo.


Ujumbe wa twitter wa Rihanna uliochapishwa siku ya Jumanne unahusishwa na habari kuhusu kuzuiwa kwa mitandao katika maeneo yenye maandamano.


India ilisitisha huduma za intaneti katika maeneo matatu mjini Delhi, ambako maelfu ya wakulima walipiga kambi kupinga sheria mpya.


Serikali ilisema kuzimwa kwa mitandao kulifanyika kwa sababu za kulinda ”usalama wa Umma”.


Maandamano hayo yalivutia vichwa vya habari kimataifa juma lililopita pale maandamano ya wakulima yalipomalizika katika mazingira ya vurugu zilizosababisha mtu mmoja kupoteza maisha na askari kadhaa kujeruhiwa.


Baadhi ya waandamanaji walivamia eneo la kihistoria la Ngome nyekundu mjini Delhi mpaka pale walipotawanywa na polisi.


Makundi ya wakulima na viongozi wa shirikisho wamekemea vurugu zilizojitokeza lakini wamesema kuwa hawatasitisha maandamano.


Ujumbe wa twitter wa mwanamuziki huyo wa pop katika ukurasa wake wenye wafuasi milioni 101 uliungwa mkono duniani.


Kulikuwa na watu wengi waliomkosoa muimbaji huyo kwa kuunga mkono maandamano dhidi ya sheria, ambazo zimetetewa na serikali na wanaoiunga mkono serikali.


Muingizaji wa kike wa filamu nchini India Kangana Ranaut, anayeunga mkono chama cha Waziri Mkuu Narendra Modi, Bharatiya Janata(BJP) alituma ujumbe ukinukuu ujumbe wa twitter.


”Hakuna anayezungumzia kuhusu hilo kwa kuwa sio wakulima, ni magaidi ambao wanataka kuigawanya India,” aliandika . Saa chache baada ya Rihana kuandika, Greta Thunberg aliandika katika ukurasa wa Twitter akiwaunga mkono wakulima.


Mpwa wa Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris pia aliweka chapisho lake akiashiria kuwa pamoja na wakulima waliokuwa wamegoma.


”Sote tunapaswa kukasirishwa na kuzimwa kwa mitandao India na vurugu zilizoelekezwa na waandamanaji wakulima,”aliandika.


Mbunge nchini Uingereza Claudia Webbe pia ameonesha kuwaunga mkono wakulima, akiandika,” Asante Rihanna. Katika kipindi ambacho utawala wa kisiasa unapungua, tunawashukuru wengine kwa kupiga hatua kwenda mbele.”


Maandamano ya wakulima, yamekuwepo kwa mwezi wa tatu sasa, yakitoa changamoto kubwa kwa Bw.Modi. Serikali ya BJP imesema itaahirisha sheria hizo lakini wakulima wametaka sheria hizo kufutwa kabisa.


Mamlaka zinakataa kukosolewa na, Jumatatu, Twitter ilirudisha akaunti kadhaa za raia wa India ambazo zilizuiwa hapo awali baada ya ilani ya kisheria ya serikali, kutoa pingamizi kulingana na utaratibu wa Umma.


Akaunti hizo zilijumuisha za viongozi wa wakulima, wanaharakati na jarida la habari.Wakulima wamepiga kambi katika mji a Delhi kwa wiki kdhaa sasa


Wakulima wamepiga kambi katika mji a Delhi kwa wiki kdhaa sasa

Sheria za kilimo zenye utata zimelegeza sheria kuhusu uuzaji, bei na uhifadhi wa mazao ya shamba ambayo yamewalinda wakulima wa India kutoka soko huria kwa miongo kadhaa.


 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

Wakulima wanahofu kuwa sheria mpya zitatishia makubaliano yaliyodumu kwa miongo -kama vile uhakika wa bei na kuzorotesha nguvu ya kujadili bei hali itakayosababisha kunyonywa na makampuni binafsi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad