Sababu za kipigo cha Tanzania kutoka Ghana

 


Timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, ilitupa karata yake ya kwanza jana jioni kwenye mchezo wa kundi C dhidi ya timu ya taifa ya Ghana na Ngarongoro Heroes ikafungwa mabao 4-0.

 

Baada ya Ngorongoro Heroes kupokea kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Ghana kwenye michuano ya AFCON kwa wachezaji chini ya umri wa miaka 20, kocha wa kikosi hicho Jamhuri Kikwelu 'Julio', amesema kutotumia nafasi vizuri za kufunga ni sababu ya kupoteza mchezo huo na ana matumaini watafanya vizuri kwenye michezo iliyosalia.


''Timu imejitahidi imecheza vizuri na kama unavyofahamu ni mara ya kwanza kushiriki mashindano haya, lakini pamoja na yote tumeweza kutawala mchezo lakini nafasi tulizozipata hatukuweza kuzitumia vizuri, lakini pamoja kuwaheshimu Ghana sio kwamba wametuzidi sanaa mpira, isipokuwa wao wamepata nafasi wametumia sisi hatukuzitumia nafasi vizuri.”


Licha ya kupoteza mchezo huo kwa idadi hiyo mkubwa ya mabao kocha Julio anaamini timu yake itafanya vizuri kwenye michezo inayofata


''Tunaamini mechi nyingine zinazokuja tutafanya vizuri hatukufanya vibaya sana vijana wangu wamefanya vizuri na nawapongeza, lakini kingine ugeni wa mashindano ndio uliochangia kupoteza kwasababu wenzetu wanauzoefu mkubwa ndio maana wameweza kuzitumia nafasi walizozipata''


Mchezo mwingine wa kundi hilo uliochezwa jana usiku na timu ya taifa ya Morocco iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Gambia. Sasa baada ya michezo hii Ghana ndio wanaongoza kundi C wakiwa na alama 3 sawa na Morocco, nafasi ya 3 Gambia na Tanzania wanaburuza mkia kutoka na kufungwa idadi kubwa ya mabao.


Na mchezo unaofaya Tanzania itashika dimbani kuminyana na Gambia utakao chezwa Februari 19, 2021, katika fainali zinazoendelea huko nchini Mouritania, kabla ya mchezo wa mwisho ambao watacheza dhidi ya Morocco Februari 22, 2021

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad